Msani maarufu wa bongo nchini Tanzania Diamond platinumz ameeleza kwamba kuwa msani tajika hauhitaji sauti nzuri tu pekee.
Diamond kwa upande wape anaamini kwamba kuwa msani ni ubunifu wa kuwaza na kujaribu kutafua mbinu mpya kila kukicha.
Amesisitiza kwamba msani anafaa kuwa na uwezo wa kuimba kwa sauti tofauti tofauti. kwa upande wake anaamini kwamba ana uwezo wa kufanya mziki wa kila aina ambao atapewa kuufanya.
"Uimbaji si sauti, ingekuwa usanii ni sauti basi Wema sepetu angekuwa msani mkubwa hapa nchini.... Mimi naweza imba base, suprano. ukinipa wimbo wowote ule mimi naimba," alisema Diamond.
Mwanamziki huyo wa Wasafi alikuwa akieleza baada ya wanahabari kumuuliza iwapo sauti yake ndio inayomfanya kuimba.
Diamond pia aliwahi kunukuliwa akisema kwamba ingekuwa uimbaji ni sauti basi msani wa Kenya Bien-Aime Baraza hangeshinda tuzo kama msani bora Afrika Mashariki.
Mwanamziki huyo wa Wasafi ni mmoja kati ya waimbaji ambao wameimba ngoma nyingi zaidi na kwa njia tofauti. Ana uwezo wa kuimba kwa kasi, mwendo wa pole. pia aliwahi kutoa kolabo na msani wa Rhumba Kofi Olomide akiimba na sauti nzito kabiza.
Kwa upande mwingine, Diamond aliwahi kuimba wimbo kwa sauti ambayo mashabiki waliikosa kwa muda uliokwenda kwa jina 'Yatapita.' Mabadiliko ya wimbo huo yalikubaliwa haraka na mashabiki hasa wale wa Afrika Mashariki ambao walikuwa wamepoteza sauti kama hio katika miziki za mwanamziki huyo.
Diamond kando na kuwa msanii wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, ni mcheza ngoma, mhisani na mfanyabiashara. Ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi Lebo, Wasafi Bet na Wasafi Media.
Diamond amepata wafuasi wengi Afrika Mashariki na Kati.] Alikuwa msanii wa kwanza wa Afrika kufikia maoni milioni 900 kwenye YouTube.